WALENGWA
NI KUANZIA:Wahitimu
Elimu ya Msingi/Sekondari /Watu wazima na watu kutoka
katika taasisi mbalimbali wanaohitaji kujiendeleza katika fani hii (KWA JINSIA ZOTE)
KOZI ZITOLEWAZO NI:
A. Umekenika
(MV. Mechanics) katika vitendo na (Nadharia)
B. Umeme wa magari (Auto electrical) katika
vitendo na (Nadharia)
Mafunzo ya ufundi:
kwa njia ya lugha ya Kiswahili bila masomo bebeshi yataendeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya hapo utafanya mtihani
wa Chuo tu kwa ajili ya kupatiwa cheti cha kuhitimu mafunzo chuoni.
Ila
unaweza kuomba kufanya Mtihani wa
Taifa wa(FANI) na
hii utaruhusiwa baada ya kuonekana rekodi zako
za mahudhurio mazuri kimasomo na katika mitihani yako ya majaribio ya kila wiki
kwa mwaka mzima, siyo vinginevyo.
Wakati
wa kuanza uje na madaftari
(2) aina ya Counter Book, Kalamu, Rula, Picha (3) Passport size.
ADA YA MASOMO KWA MWAKA NI TSH.
490,000/= tu
A. Mwanachuo anapoanza masomo zilipwe
Tshs. 100,000/= ada ya awali, na
Tshs.20,000/=
za uniform na kitambulisho kwa mwaka mzima.
B. Pasipo kulipa malipo kamili ya Tsh.
120,000/= kama ilivyoelekezwa wakati wa kuanza masomo utalazimika kuijaza fomu ya mkataba ambayo utaigharamia Tshs 5000/= na utapewa muda wa siku saba kumalizia kiasi kilichobaki
C .Salio la kiasi cha Tsh. 390,000/=
zitakuwa zinalipwa kwa awamu kisi cha
Tsh.17,000/=
kwa
mujibu wa maelekezo ya fomu ya malipo
MAFUNZO YA UFUNDI KWA NJIA YA MFUMO WA CBET
Mafunzo
ya ufundi kwa njia
ya mfumo wa CBET (Kitaifa)
yataendeshwa kwa lugha ya kingereza
kwa kipindi cha miaka miwili ndipo utaruhusiwa kufanya mtihani wa Taifa. Hii nikutokana
na maelekezo ya mtahala wa ufundishaji kitaifa (VETA) na ni lazima uyasome masomo bebeshi kama ifuatavyo:-
|
Ada ya masomo kwa mwaka ni Tshs. 1,400,000/=
unapoanza zilipwe Tshs. 700,000/=salio la kiasi cha Tshs. 700,000/= zitalipwa kwa awamu kiasi Tshs. 70,000/= kila mwisho wa mwezi hadi mwisho wa malipo. Wakati wa kuanzia masomo ya ufundi uje na madaftari ya masomo yote yaliyohainishwa katika kipengele namba (4) na picha (3) passport size.
MALIPO
Malipo
yote yalipiwe katika Bank zilizoelekezwa,
hii ni kwa usalama wa fedha yako. Hakikisha unaandika jina la Mwanachuo
katika Pay - in slip ya Bank na uilete Chuoni kwa uthibitisho wa malipo. Bank zinazohusika ni:-
A. CRDB popote Tanzania Account
Na. 01J1008454800 - Bruno Auto Training Centre
B. AKIBA Commercial Bank Tawi la
Buguruni au popote. Account Na. 10200586487 - BRUNO V.T.C